Ripoti kutoka Iraq zinasema kuwa
vikosi vya serikali pamoja na wanamgambo wa kishia wameyateka baadhi ya
maeneo yaliodhibitiwa na wapiganaji wa kisunni kazkazini mwa Baghdad
mbali na miji kadhaa kutoka kwa waasi hao.
Hatahivyo miji ya Tikrit na Mosul bado imesalia chini ya udhibiti wa wapiganaji hao .Maafisa wamesema kuwa shambulizi hilo ni la makosa.
Waziri wa maswala ya kigeni nchini Marekani John Kerry awali aliiambia serikali ya Iraq kwamba usaidizi wa Marekani katika kukabiliana na wanapiganaji wa jihadi wa ISIS utafanikiwa iwapo viongozi wa Iraq wako tayari kuwacha tofauti zao.
Marekani inapeleka meli ya kubeba ndege katika eneo la Ghuba ili kukabiliana na ghasia nchini humo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni