KOCHA
Oscar Tabarez amesme kwamba Luis Suarez amefanywa mbuzi wa kafara na
FIFA wakati akizunguma na Waandishi wa Habari Maracana jioni ya jana.
Tabarez
alisoma taarifa aliyoandaa kwa dakika 13 akisema kwamba, presha ya
vyombo vya habari Uingereza baada ya kumng'ata beki wa Italia, Giorgio
Chiellini Jumanne iliyopita ndiyo imeisukuma FIFA kumfungia kwa miezi
minne.
Kocha
huyo wa Uruguay kisha mara moja akatangaza kujiuzulu wadhifa wake
katika Kamati ya Ufundi wa FIFA na amemuambia Suarez kwamba
anaungwa mkono na wananchi wake wa Uruguay.
Sapoti: Luis Suarez akiwa ameba mwanawe wa kike wakati akiwapungia mkono mashabiki nje ya nyumbani kwake, Montevideo
Tabarez
amesema: "Mara nyingi unasahau kwamba, mbuzi wa kafara ni ambaye ana
haki na haswa katika kesi mahsusi kama hii, mbali na makosa na faulo
aliyocheza, ametoa mchango uwanjani. Ni mchango ambao unatolewa na
wachezaji wakubwa duniani.
"Tunafahamu
itifaki na si kwa sababu ya wasifu wake, kwa sababu ya makosa, lakini
ana upande mwingine naye. Huo ni ujumbe: Adhabu imezidi mno. "Kama
kocha na profesa, na mwalimu wa zamani, nawasilisha nadharia ya mbuzi
ya kafara. Unajua nazungumzia nini, utoaji wa adhabu, kwa mtu ambaye
amefanya kosa, si uhalifu.
"Natumaini
nina jibu, lakini kama watu wengi, ambao tu hawawezi kufanya maamuzi ya
kinidhamu - mani ameshindsa? Nani ameshindwa? Nani amenufaika? Nani
ameuawa? Nani ameula upande wake?
"Kwa
moja ya maswali hayo, sitakupa jibu la mwisho, lakini nitatafuta
majibu. Adhabu waliyotoa katika maamuzi yao, inatia shaka. Baada ya
tukio la Suarez na Chiellini tumeona mengi yaliyoibuka.
"Tunatakiwa kutoa adhabu na vikwazo, lakini jambo moja la lazima ni kusikiliza kutoka kwa muhusika.’
Tabarez
aliikandia vikali Kamati ya Nidhamu ya FIFA baada ya kushindwa kumpa
Suarez nafasi ya kujitetea baada ya tukio dhidi ya Chiellini.
Anasafisha meno: Suarez akiwa amejiangusha chini baada ya kumng'ata Chiellini
Tukio: Suarez akimng'ata Chiellini began katika mchezo ambao Uruguay iliifunga 1-0 Italia
Kocha
huyo wa Uruguay, anajiandaa kwa mchezo wa leo dhidi ya Colombia Uwanja
wa Maracana, hatua ya 16 Bora Kombe la Dunia amewataka wananchi wa nchi
yake kupinga uamuzi huo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni