Jembe Jipya! Luke Shaw akiwa na jezi mpya ya klabu yake ya Manchester United |
Ander Herrera alipotangazwa ramsi kujiunga kwa Mashetani Wekundu |
MABINGWA
wa zamani wa England, Manchester United imezidi kuimarisha kikosi chake
baada ya kufanikiwa kumsainisha beki wa kushoto wa Southamptom na timu
ya taifa ya nchi hiyo iliyotolewa kwenye Kombe la Dunia, Luke Shaw.
Kwa mujibu wa duru za kandanda za
England zinasema kuwa, Mashetani Wekundu hao wamekamilisha uhamisho wa
Shaw kwa gharama za Pauni
Milioni 31.5 kwa mkataba wa miaka minne.rd.
Mchezaji
huyo amekamilisha vizuri vipimo afya katika Uwanja wa mazoezi wa
United, Carrington na ameambiwa atakuwa beki wa kushoto chaguo la kwanza
la kocha Louis van Gaal.
Inafahamika
amehakikishiwa namba na beki mkongwe mwenye umri wa miaka 33, Patrice
Evra, ambaye atabakia United, anatarajiwa kupunguziwa majukumu klabuni
hapo.
Usajili wa Shaw umekuja siku moja baada
ya klabu hiyo kufanikiwa kunyakua Ander Herrera kutoka Athletic Bilbao
kwa ofa ya pauni milioni 29.
Man United ilikuwa na msimu mbaya ligi
iliyopita chini ya kocha David Moyes ambaye alitimuliwa na nafasi yake
kushikiliwa kwa muda Ryan Giggs kabla ya Luis van Gaal kupewa kibarua
cha kuwa kocha mkuu sasa.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni