WACHEZAJI
watatu akiwemo winga kutoka akademi ya Orlando Pirates ya Afrika
Kusini, Gery Epeso wametua klabu bingwa ya Tanzania Bara, Azam FC kwa
ajili ya majaribo.
Kocha Mcameroon Joseph Marius Omog amewapokea wachezaji hao mazoezini na amesema atahitaji kuwaangalia kabla ya kuamua.
“Wakati mwingine unaweza kupata mchezaji mzuri kati ya hawa ambao wanakuja majaribio, acha tuwaangalie kwa muda,”alisema.
Kocha Mcameroon Joseph Marius Omog amewapokea wachezaji hao mazoezini na amesema atahitaji kuwaangalia kabla ya kuamua.
“Wakati mwingine unaweza kupata mchezaji mzuri kati ya hawa ambao wanakuja majaribio, acha tuwaangalie kwa muda,”alisema.
Gery Epeso ametua majaribio Azam FC |
Epeso ameiambia BIN ZUBEIRY leo kwamba alikuwa anachezea akademi ya Orlando, lakini kwa sasa ni mchezaji wa klabu ya Don Bosco ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) ambako ndiko nyumbani kwao.
Mbali na winga huyo wa kushoto, wachezaji wengine waliotua kujaribu bahati yao Azam FC ni mshambuliaji Hisham Abdallah aliyekuwa anacheza soka ya kulipwa Hungary na kiungo mkabaji, Athumani Ali Sheikh kutoka IFK Amal ya Daraja la Pili Sweden.
Hisham anayecheza zaidi kama mshambuliaji wa pili, asili yake ni Zanzibar wakati Sheikh ni mwenyeji wa Dar es Salaam.
Hisham Abdallah ametokea Hungary |
Athumani Sheikh ametokea Sweden |
Tayari Azam FC ina wachezaji watano wa kigeni ambao ni kiungo Kipre Michael Balou, washambuliaji Kipre Herman Tchetche wote kutoka Ivory Coast, Didier Kavubangu kutoka Burundi, Ismaila Diara kutoka Mali na Brian Umony kutoka Uganda.
Hata hivyo, kuna uwezekano Umony akatemwa na nafasi yake akapewa mchezaji mwingine- maana yake Epeso kama atamvutia kocha Omog anaweza kuziba nafasi ya Mganda huyo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni