Mkazi wa Mwananyamala, Amina Maige(42) anayetuhumiwa kumng'ata mfanyakazi wake wa ndani, amepandishwa kizimbani kusomewa maelezo ya awali baada ya upelelezi wa kesi hiyo kukamilika.
Amina alisomewa maelezo hayo jana katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kinondoni mbele ya Hakimu Yohana Yongolo.
Wakili wa Serikali Tumaini Msikwa alidai kati ya Januari na Juni mwaka huu, maeneo ya Mwananyamala Wilaya ya Kinondoni, Maige alimng'ata Yusta Kashinde(20) sehemu mbalimbali za mwili wake na kumsababishia maumivu.
Mshitakiwa alikana maelezo aliyosomewa na kwamba aliiomba mahakama kumpatia dhamana.
Wakili M
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni