Mkurugenzi wa Bin Slum Tyres, Nassor Bin Slum
(kulia) na katibu mkuu wa Ndanda FC , Edmund Kunyengana (kushoto)
wakitia sahihi mkataba wa udhamini.
Wakibadilishana mkataba
BAADA ya kusaini mkataba na Mbeya City
pamoja na Stand United kampuniI ya Bin Slum Tyres Limited, imesaini Mkataba wa
udhamini na Ndanda FC ya Mtwara leo jijini Dar es salaam.
Mkurugenzi wa kampuni hiyo, Nassor Bin
Slum amesema kuwa wameingia Mkataba wa mwaka mmoja na Ndanda wenye thamani ya
Sh. Milioni 50.
Hii ndio jezi yenye nembo ya Bin Slum
itayotumika msimu ujao.
Katika mkataba huo, Bin Slum amesema
kwamba, Ndanda watavaa jezi zenye nembo ya matairi ya Vee Rubber kwa mbele
pamoja na kuweka mabango ya bidhaa hizo kwenye mechi zao za nyumbani, Uwanja wa
Nangwanda Sijaona.
Katibu Mkuu wa Ndanda FC, Edmund Kunyengana Njowoka amesema udhamini hauo utawasaidia kufanya vizuri Ligi Kuu.
Katibu Mkuu wa Ndanda FC, Edmund Kunyengana Njowoka amesema udhamini hauo utawasaidia kufanya vizuri Ligi Kuu.
Kitu `Mtwara Kuchele`, Bin Slum imeamua kuidhamini
timu mpya wa Ndanda fc. Kulia ni Mkurugenzi wa Bin Slum Tyres, Nassor Bin Slum
na katibu mkuu wa Ndanda FC , Edmund Kunyengana (kushoto)
wakiwaonesha jezi waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam (hawapo
pichani).
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni