STAY WITH US

LightBlog

Breaking

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

CHANZI OPEN SCHOOL

CHANZI OPEN SCHOOL

Alhamisi, 5 Juni 2014

STARS KUINGIA KAMBINI JUNI 11 KUKUSANYA NGUVU ZA KUUA MAMBA

Na Boniface Wambura, DAR ES SALAAM
TIMU ya soka ya taifa Tanzania, Taifa Stars itaingia tena kambini Jumatano (Juni 11 mwaka huu) ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya mechi ya raundi ya pili ya michuano ya Afrika dhidi ya Msumbiji itakayochezwa Julai 20 mwaka huu jijini Dar es Salaam.

Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager itakuwa na kambi ya siku tatu jijini Dar es Salaam ikijumuisha wachezaji 28. Kwa mujibu wa programu ya Kocha Mart Nooij, Stars itaingia tena kambini Juni 24 mwaka huu.
Taifa Stars itaingia kambini Juni 11 kuanza maandalizi ya mechi na Msumbiji

Wachezaji wanaotakiwa kuripoti kambini ni Deogratias Munishi, Aishi Manula, Benedictor Tinoko, Kelvin Yondani, Said Moradi, Nadir Haroub, Joram Nason, Shomari Kapombe, Oscar Joshua, Edward Charles, Aggrey Morris na Pato Ngonyani.
Wengine ni Mwinyi Kazimoto, Frank Domayo, Amri Kiemba, Erasto Nyoni, Jonas Mkude, Said Juma, Haruna Chanongo, Himid Mao, Said Ndemla, John Bocco, Simon Msuva, Kelvin Friday, Ramadhan Singano, Khamis Mcha, Mrisho Ngasa na Mwegane Yeya.
Wakati huo huo: Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limepokea taarifa za kutolewa wito bungeni wa kulitaka litumie tiketi za elektroniki katika kukusanya mapato.
“Tunataka ieleweke wazi kwa umma wa Watanzania kuwa si nia yetu kuchelewesha matumizi ya uingiaji mpirani kwa tiketi za elektroniki. Ieleweke
kuwa mfumo wa kuingia kwenye mbuga, KCMC, mipakani ni tofauti na uingiaji mpirani,”.
“Katika mpira wa miguu wanaingia maelfu ya watu katika kipindi kifupi. Kwa kuzingatia umuhimu wa kulinda usalama wa watazamaji na miundombinu ya viwanja ndio maana tulisitisha matumizi ya tiketi za elektroniki hadi tujihakikishie usalama wa matumizi yake,”.
“Tunafanya jitihada kwa karibu na mzabuni benki ya CRDB ili kuhakikisha mfumo huu unaanza kutumika mara moja. Kwa niaba ya sekta ya michezo tunatoa wito kwa Serikali kushusha au kuondoa kodi kubwa zinazotozwa kwenye vifaa vya michezo, hasa vinavyotumiwa na watoto kuanzia umri wa miaka 6-12, ili watoto wetu waweze kuvipata kirahisi toka kwa wazazi wao ili waweze kujifunza kucheza michezo kisasa tangu wakiwa wadogo,”imesema taarifa ya TFF.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA

Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...

TIBA YA KIIMANI

TIBA YA KIIMANI

a

a
Adbox