SHIRIKISHO
la Soka la Kimataifa (FIFA) limemuondoa nyota wa Uruguay, Luis Suarez
kwenye michuano ya Kombe la Dunia na kufungiwa pia kucheza Ligi Kuu ya
England hadi mwishoni mwa Oktoba.
Amekiona cha moto: Nyota wa Uruguay, Luis Suarez ameadhibiwa na FIFA kwa kumng'ata beki wa Italia
Kamati
ya Nidhamu ya FIFA, baada ya kikao chake cha zakdi ya saa 10 usiku wa
jana na leo asubuhi, imemfungia Suarez mechi tisa za mashindano za ya
kimataifa na miezi minne jumla kutojihusisha kabisa na soka.
Hiyo
inafuatia mshambuliaji huyo kumng'ata began beki wa Itakia Giorgio
Chiellini, Uruguay ikiibuka na ushindi ulioivusha hatua ya 16 Bora- hiyo
ikiwa ni mara ya tatu kwa mchezaji huyo kufanya hivyo.
Suarez atakosa mechi 13 za Liverpool ingawa haiwesi kuathiri mazungumzo yoyote ya kuuzwa na ametozwa faini ya Pauni 65,000.
Rais wa Chama cha Soka Uruguay, Wilmar Valdez amethibitidha watakata rufaa kupinga adhabu ya Luis Suarez aliyopewa na FIFA.
Wadhamini wa mshambuliaji huyo, adidas wan a mazungumzo ya dharula juu ya mustakabali wao kwa mchezaji huyo.
Uruguay
inajiadaa kwa rufaa, lakini wazi Suarez atakosa mchezo wa kesho wa
hatua ya 16 Bora dhidi ya Columbia Uwanja wa Maracana Stadium.
MECHI ZA LIVERPOOL ATAKAZOKOSA SUAREZ
Agosti 16: Liverpool v Southampton
Agosti 23: Manchester City v Liverpool
Agosti 30: Tottenham Hotspur v Liverpool
Septemba 13: Liverpool v Aston Villa
Septemba 16: Champions League matchday 1
Septemba 20: West Ham United v Liverpool
Septemba 27: Liverpool v Everton
Septemba 30: Champions League matchday 2
Oktoba 4: Liverpool v West Bromwich Albion
Oktoba 18: Queens Park Rangers v Liverpool
Oktoba 21: Champions League matchday 3
Oktoba 25: Liverpool v Hull City
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni