MSHAMBULIAJI
Luis Suarez anakabiliwa na adhabu kali baada ya nyota huyo wa Liverpool
kumng'ata beki wa Italia, Giorgio Chiellini began jana Uruguay
ikishinda 1-0 katika mchezo wa mwisho wa Kundi D Kombe la Dunia nchini
Brazil.
Ona hapa: Chiellini akionyesha sehemu ambayo aling'atwa na meno na Suarez
Kwa
mara ya tatu akifanya kosa la ajabu kihistoria, mchzaji huyo mwenye
umri wa miaka 27 alinaswa na kamera
akimtia meno mchezaji mwenzake begani.
akimtia meno mchezaji mwenzake begani.
Hata
hivyo, baada ya mechi hodari huyo wa kufunga mabao alijitetea akisema:
"Hayo mambo yanatokea ndani ya boksi. Tulikuwa tunapambana, kifua dhidi
ya bega nami nikapata pigo jichoni,".
Chiellini
kwa upande wake amesema: "Suarez amefanya hivyo na anaweza kuepuka
adhabu kwa sababu FIFA inataka nyota wake wabaki katika Kombe la Dunia.
Ningependa kuona wanatumia video ya ushahidi dhidi yake. Refa aliona
alama ya kung'atwa, pia, lakini hakufanya lolote juu ya hili,".
FIFA imesema itachunguza tukio hilo leo baada ya refa wa Mexico, Marco Rodriguez kutona wakati linatokea.
Bodi
hiyo ya soka duniani hapana shaka itamchukulia hatua kali Suarez,
ikizingatia makosa yake ya kihistoria ya utovu wa nidhamu.
Wana
nguvu ya kumfungia hadi miaka miwili kama wataona inastahili. Inaweza
kuwa Suarez atafungiwa mecnhi kadhaa, ambazo zitamfanya awe amemaliza
kucheza Kombe la Dunia mwaka huu, Uruguay ikiwa imefuzu 16 Bora baada ya
kuitoa Italia.
Maji moto: Luis Suarez akisafisha meno yake baada ya kumng'ata Giorgio Chiellini
Picha
za bega la beki Chiellini zinaoneysha dhahiri alama ya meno baada ya
Mtaliano huyo kuteremsha jezi yake kuonyesha ushahidi wa tukio hilo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni