kiisilamu
Inaripotiwa kuwa wanawake pamoja na wasichana sitini walitekwa nyara Kaskazini Mashariki mwa Nigeria wiki iliyopita.
Ripoti
zilizotolewa mwishooni mwa wiki iliyopita zilisema kuwa ishirini kati
yao walichukuliwa na kundi linaloaminika kuwa Boko Haram.
Wanawake hao walitekwa wakati wa uvamizi uliofanywa katika vijiji vilivyo katika wilaya ya Damboa katika jimbo la Borno.Wanawake hao inaarifiwa walitekwa nyara katika eneo la vijijini ambakop mawasiliano ni magumu sana , sababu ya kupata habari hizi kuchelewa.
Watu wanaotoroka vijiji ambavyo vilishambuliwa, wanasema kuwa wanawake na wasichana sitini walitekwa nyara wiki jana.
Baadhi
ya watoto waliotekwa ni wadogo sana wa umri. Moja ya vijiji
vilivyoshambuliwa ni kile cha Kummabza kilicho katika eneo la Damboa
katika jimbo la Borno.
BBC
hata hivyo haijaweza kuthibitisha idadi kamili ya watu waliotekwa
nyara. Hali hii imefanywa kuwa ngumu'kwani maafisa wa eneo hilo bado
hawajatoa tamko lolote kuhusu kisa hiki labda kutokana na hofu juu ya
maisha yao.
Sio
jambo la kushangaza kwamba tangu kutekwa nyara kwa wasichana miambili
wa shule kutoka Chibok , wanawake wengine wametekwa nyara
Vijiji
vingi katika eneo la Kaskazini mwa Nigeria, vinakumbwa na utovu wa
usalama na wakati ambapo Boko Haram wanapofanya shambulizi,wao huchukua
muda mrefu wakifanya uporaji na mauaji.
Mwishoni mwa wiki, idadi kubwa ya watu waliuawa karibu na eneo la Chibok.
Zaidi ya wasichana 200 wa shule walitekwa nyara eneo la Chibok mwezi Aprili.
Walitekwa nyara kutoka shule yao ya mabweni na wapiganaji wa Boko Haram.
Serikali ya Nigeria imekuwa chini ya shinikizo kali za kuitaka ifanye jitihada za kuwaokoa wasichana hao.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni