Hili ni
bomu ambalo jioni ya June 16 2014 kwenye kijiji cha Mdui kata ya Mawala
wilaya ya Mtwara vijijini kwenye mkoa wa mtwara liliokotwa na watoto
waliokua wakicheza karibu na eneo la makaburi.Taarifa ilitolewa Polisi
baadae ambapo baada ya wataalamu kuja na kuchunguza waligundua ni bomu
la kurusha kwa mkono ambalo lina namba TNT MORTAR BOMB 60MM,LOT SOL 618
ambapo Polisi kwa kushirikiana na Jeshi la Wananchi walichukua hatua za
kiusalama na kwenda kulilipua porini.
Kaimu kamanda wa Polisi Mtwara Maisha Maganga ameongea na na
kusema ‘ukiliangalia ni bomu ambalo ni la muda mrefu nadhani ni kipindi
kile cha vita ya Msumbiji, tulilipeleka porini likalipuliwa na ulipuaji
wake haukuwa na madhara… na sio kwamba ni bomu tunaweza kusema
limeletwa ama imekuaje, ni bomu la muda mrefu tu’
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni