WAKATI Robin
van Persie anafunga bao bora la kichwa katika ushindi mkubwa wa mabao
5-1 dhidi ya mabingwa watetezi wa kombe la dunia, Hispania, hakujua kama
amefanya kitu cha ajabu katika mashindano hayo.
Bao hilo la kichwa limekuwa gumzo katika mitandao ya kijamii hususani Twita.
Mashabiki wengi wa Uholanzi wakiwa
katika bustani zao kwa mapumziko, wanaigiza namna mshambuliaji huyo wa
Manchester United alivyopaa juu na kupiga kichwa na kufunga bao la bora
zaidi mpaka sasa.
Shabiki wa Uholanzi akiwa amevalia jezi yake ya rangi ya machungwa akiigiza namna Van Persie alivyofunga bao la kichwa.
Anakopi: shabiki akijaribu kuigiza staili ya ufungaji ya Van Persie kwenye mechi dhidi ya Hispania.
Hispania walishinda kombe la dunia
mwaka 2010 kwa kuwafunga Uholanzi kwenye mchezo wa fainali, lakini
safari hii mambo yamekuwa balaa.
The flying Dutchman: Van Persie aliifungia Uholanzi bao la kusawazisha
Van Persie akikimbia kumfuata kocha wa Manchester United, Van Gaal ili washangilie bao hilo.
Kula tano: Van Gaal na Van Persie wakishangilia bao pamoja na wanatarajia kukutana Old Trafford baada ya kombe la dunia.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni