Baadhi ya warembo watakaochuana kuwania taji la Miss Ubungo siku ya Ijumaa wakiwa katika pozi |
JUMLA ya warembo 18 wanatarajiwa
kuchuana kuwania taji la shindano la urembo la Miss Ubungo
litakalofanyika siku ya Ijumaa kenye ukumbi wa Land Mark Hotel, jijini
Dar es Salaam.
Aidha wadhamini zaidi wamejitokeza kudhamini shindano hilo ikiwamo kampuni ya Prima Total Hair iliyojitoikeza kuwadhamini washindi watatu wa shindano hilo.

Jumamosi iliyopita Kampuni hiyo
liwamwagia sifa wanyange watano waliopita katika kumtafuta Miss Talent
katika ukumbi wa Club Maisha uliopo Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa Meneja Masoko wa Kampuni hiyo Idd Gubwe alisema,"Wanyange wote waliohusika katika kinyang'anyiro cha kumtafuta Miss Talent wanaonekana kuwa na mvuto zaidi hivyo kwa maono ya haraka haraka shindano hilo litakuwa na ugumu kwa wanyange hao katika siku hiyo ya Ijumaa,"alisema Gubwe.
Gabwe alisema tunaamini kwa mtazamo wetu mshindi atapatikana mwenye mvuto na vigezo na hivyo udhamini wetu kuonekana bora katika safari ya mafanikio ya ulimbwende nchini.
Kwa mujibu wa muandaaji wa shindano hilo, Sam Sammi ni kwamba kampuni hiyo imeahidi kutoa zawadi ya Sh. 450,000 kwa mshindi wa kwanza, Sh 300, 000 kwa mshindi wa pili na Sh. 250,000 kwa mshindi wa tatu na imesema inaweza kuongeza udhamini zaidi kabla ya fainali hizo za Ijumaa.
Sammi alisema hadi sasa jumla ya wanyange 18 wamekuwa wakijifua kwenye mazoezi yanayoendelea katika ukumbi wa Ako Labamba Club uliopo Urafiki jijini Dar es Salaam tayari kwa kinyang'anyiro hicho.
Mratibu huyo aliwataja baadhi ya warembo hao watakaochuana katika shindano hilo maarufu kama Redd';s Miss Ubungo ni pamoja na Rachel Steven, Nancy Mella, Zubeda Hussein, Nurinah Mkindo, Annastazia John,Queen Joel Mtui, Grace John Mrema, Aisha Saleh na Beatrice Kaiza.

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni