Mabingwa wa Bara, Azam FC watashiriki Kombe la Kagame |
BARAZA la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) limeiongeza Azam FC katika michuano ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Kagame Cup inayotarajiwa kufanyika mwezi ujao mjini Kigali, Rwanda.
Chanzo cha Habari cha uhakika kutoka makao makuu ya CECAFA, Nairobi, Kenya kimeiambia BIN ZUBEIRY kwamba, Azam imeongezwa kuchukua nafasi ya timu iliyoshindwa kuthibitisha kushiriki michuano hiyo.
Chanzo hicho kimesema sababu ya kufikiriwa Azam kwanza ni kutokana na kwamba ilistahili kucheza michuano mipya ya CECAFA, Nile Basin Mei mwaka huu, lakini ikashindwa kwa sababu ilikuwa imekwishavunja kambi yake na kuwaruhusu wachezaji wake kwenda likizo.
Nafasi
ya Azam FC katika michuano hiyo inayoshirikisha mabingwa wa Kombe la FA
au washindi wa pili wa Ligi Kuu za nchi wanachama wa CECAFA
iliyofanyika kwa mara ya kwanza mwaka huu Sudan, ilichukuliwa na Mbeya
City.
“Lakini pia kama utajua, Tanzania haikushiriki Kombe la Kagame mwaka jana baada ya Serikali yake kuzuia timu kwenda Sudan, CECAFA pia imezingatia hilo kuipa nafasi hiyo ya upendeleo Tanzania,”kimesema chanzo hicho.
Waliokuwa mabingwa watetezi wa Kagame, Yanga SC na mabingwa wa Bara 2012, Simba SC walishindwa kwenda Sudan mwaka jana kwa kuhofia mapigano ya wenyewe kwa wenyewe yaliyokuwa yakiendelea nchini humo na Vital’O ya Burundi ikachukua Kombe.
“Tuliwaandikia Azam kuwapa mwaliko, na wametujibu na kututhibitishia watashiriki, ni nzuri sana na ratiba ikitoka na wao watakuwamo,” kimesema chanzo hicho.
Tanzania sasa itakuwa na wawakilishi kwenye michuano ya Sudan, mabingwa wa Bara mwaka jana Yanga SC na mabingwa wa msimu huu, Azam FC ambao walikutana kwenye fainali ya michuano hiyo mwaka 2012 mjini Dar es Salaam. Yanga ilishinda 2-0 chini ya kocha Mbelgiji, Tom Saintfiet na kutwaa Kombe.

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni