Kabwaga: Fred alikuwa mbuzi wa kafara kwa mashabiki katika hatua ya mwisho ya mashindano.
Fred amestaafu soKa la kimataifa baada ya Brazil kuharibu mno katika fainali za kombe la dunia ndani ya ardhi yake mwaka huu.
Mshambuliaji huyo mwenye miaka 30 ambaye
ameichezea nchi yake mechi 39, amekuwa mbuzi wa kafara kwa mashabiki wa
Brazil waliomkosoa kuonesha kiwango cha chini.
Brazil ilifungwa mabao 7-1 na Ujerumani
katika mchezo wa nusu fainali jumanne ya wiki iliyopita na juzi jumamosi
walifungwa mabao 3-0 na Uholanzi katika mchezo wa mshindi wa tatu.
Fred alikuwa mfungaji bora wa mashindano ya kombe la bara mwaka jana ambapo Brazil iliibuka mabingwa.
Fred kila alipogusa mpira katika kipigo cha mabao 7-1 dhidi ya Ujerumani, Belo Horinzote alikumbana na kelele za kuzomewa.
Hatua hii ya kustaafu imekuja baada ya
mwaka mmoja tu kupita tangu mshambuliajia huyu wa Fluminense ashinde
kiatu cha mfungaji bora wa kombe la mabara akiwa na mabao matano.
Fred alifunga bao lake la kwanza katika
mechi ya kirafiki ya Brazil dhidi ya UAE ambapo wazee wa samba
walishinda mabao 8-0 mwaka 2005.
Rekodi nzuri: Fred ameichezea Brazil mechi 39 na kufunga mabao 18 tangu 2005.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni