Scolari alijiuzulu baada ya Brazil kufungwa 7-1 na Ujerumani Kombe la Dunia
SHIRIKISHO
la Soka Brazil (CBC) limeteua Dunga kuwa kocha mpya wa timu ya taifa
leo, wiki mbili baada ya kipigo cha ainu cha mabao 7-1 kutoka kwa
Ujerumani kwenye Nusu Fainali ya Kombe la Dunia, kilichomfanya kocha
Luiz Felipe Scolari abwage manyanga.
Mwalimu
huyo mwenye umri wa miaka 50, aliyekuwa nahodha wa kikosi cha Brazil
kilichotwaa Kombe la nne la Dunia mwaka 1994, mara ya mwisho alikuwa
kocha wa timu hiyo mwaka 2010 alipofukuzwa baada ya timu kutolewa katika
Robo Fainali ya Kombe la Dunia Afrika Kusini.
"Nina furaha kurejea,"aliwaambia Waandishi wa Habari.
Aliiongoza Brazil
hadi Robo Fainali ilipotolewa kwa kipigo cha mabao 2-1 kutoka kwa
Uholanzi, lakini akalaumiwa kwa mbinu zake mbovu na kufukuzwa na nafasi
yake kuchukua Mano Menezes.
Awali
aliiwezesha timu hiyo kushinda mechi 42, ndani take akitwaa mataji ya
Copa America mwaka 2007 na Kombe la Mabara mwaka 2009, akipoteza mechi
sita tu kati 60.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni