Kocha Mkuu wa Simba, Zdravko Logarusic amesema anataka
kuwa na furaha na hakuna kitakachomfurahisha zaidi ya kuona kikosi chake
kinashinda.
Loga raia wa Croatia amesema anataka kuwa na
maandalizi ya uhakika katika kipindi cha sasa kwa kuwa ndiyo muhimu kumpatia
ushindi.
“Ukikosea katika kipindi cha mwanzo, basi ujue una
kazi ngumu. Furaha ya kufanya vizuri ni jambo jema kwa kocha yoyote.
“Natamani kushangilia kila wakati, lakini najua furaha
itapatikana kama nitafanya mambo ya uhakika sasa na wachezaji wanapaswa
kujituma na kunivumilia,” alisema Logarusic.
Tayari Loga ametua jijini Dar es Salaam na anaanza
kazi kesho kwenye viwanja vya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kujiandaa na msimu
mpya wa 2014-15.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni