MENEJA MPYA Louis van Gaal amesema kwanza anafanya tathmini ya Kikosi
cha Manchester United kilichopo kwa Muda wa Wiki 4 kisha ataamua kama
watanunua Wachezaji wapya.
Van Gaal, akiongea na Wanahabari kwa mara ya kwanza kufatia utambulisho wake kama Meneja mpya, amesema yeye ndie alibariki kununuliwa kwa Wachezaji wapya Luke Shaw na Ander Herrera.
Kwa sasa kazi iliyopo mbele yake ni kutathmini Kikosi wakati kikijitayarisha kwa ajili ya Msimu mpya na amesema: “Nataka kuwaangalia Wachezaji waliopo kwa sasa. Nawajua hawa Wachezaji lakini sijawapa Mazoezi na kuwafundisha. Itachukua Wiki 3 au 4 kuona nini wanaweza kufanya kabla kununua Wachezaji wapya.”
VAN GAAL-Mataji yake:
-Ubingwa wa Ligi: Ajax (1993-94, 1994-95, 1995-96), Barcelona (1997-98, 1998-99), AZ Alkmaar (2008-09), Bayern Munich (2009-10)
-UEFA CHAMPIONZ LIGI: Ajax (1994-95)
-UEFA CUP: Ajax (1991-92)
Hata hivyo Van Gaal alikataa kuweka ahadi yeyote kuhusu Watu watarajie nini ingawa aliweka bayana Manchseter United ni ‘Klabu kubwa Duniani.’
Ameeleza: “Nitafanya juhudi zangu zote na hilo ndio naweza kutoa. Siwezi kubashiri kwa sababu hatujui. Hii ni Klabu kubwa kabisa Duniani na nimejua hilo baada ya Siku mbili tu.”
Aliongeza: “Inabidi nibadilike kwa ajili ya Klabu hii. Si rahisi lakini nitafanya juhudi zote. Ukiangalia maisha yangu ya kazi, utaona nini nimeshinda na hilo pekee ndio naweza kusema. Huko mbele tutaona kama naweza kufanya tena.”
“Ni changamoto kubwa kwa sababu ya matumaini. Nimefanya kazi Barcelona, kwa maoni yangu, Nambari Wani huko Spain. Nimeifundisha Ajax, Nambari wani huko Netherlands, Nimeifundisha Bayern Munich, Nambari wani huko Germany na sasa Man United, ambao ni Nambari Wani hapa England na natumaini kutimiza matarajio!”
Hapo kesho, Ijumaa, Louis van Gaal ataruka na Kikosi cha Man United kwenda kupiga Kambi huko California na kucheza Mechi yao ya kwanza hapo Julai 23 dhidi ya Los Angeles Galaxy.
USA-ZIARA YA KABLA MSIMU MPYA:
[Zote Nchini Marekani]
**Saa za Bongo
Jumatano 24 Julai 2014, Rose Bowl, Pasadena
0606 Manchester United v LA Galaxy
Chevrolet FC Cup
Jumamosi 26 Julai 2014, Sports Authority Field, Denver
2306 Manchester United v AS Roma
International Champions Cup
Jumanne 30 Julai 2014 [Usiku wa 29 kuamkia 30], FedEx Field, Washington DC
0230 Manchester United v Inter Milan
International Champions Cup
Jumanne 02 Agosti 2014, Michigan Stadium, Ann Arbor
2306 Manchester United v Real Madrid
International Champions Cup
Jumanne 12 Agosti 2014, Old Trafford
REUNITED14
2130 Manchester United v Valencia

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni