STAY WITH US

LightBlog

Breaking

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

CHANZI OPEN SCHOOL

CHANZI OPEN SCHOOL

Jumamosi, 12 Julai 2014

SIMBA YAAMUA KUACHANA NA STRAIKA WA HARAMBEE STARS

KIONGERA  AKIITUMIKIA KENYA KATIKA MECHI DHIDI YA MISRI.

Kamati ya usajili ya Simba imeamua kuachana na mshambuliaji Modo Kiongera anayekipiga KCB na timu ya taifa ya Kenya, Harambee Stars.

Uamuzi huo unatokana na Simba kukasirishwa na kitendo cha Kiongera kuongeza bei ya usajili katika hatua za mwisho, tofauti na walivyokubaliana awali.

Habari za uhakika kutoka ndani ya Simba zimeeleza, Kiongera alibadilika na kutaka fedha nyingi zaidi ya zile walizokubaliana na Simba.

“Kweli kama imeamua kuachana naye, maana awali makubaliano yalikuwa achukue kiasi fulani na akakubali kuja Dar, lakini mwishoni ameamua kubadilika na anataka zaidi,” kilieleza chanzo.

Kiongera alikuwa kati ya chaguo la Kocha Zdravko Logarusic ambaye alimtaka kwa kuwa amewahi kufanya naye kazi wakiwa Gor Mahia ambako alicheza baada ya kutoka kwa mkopo KCB.

Simba ilikuwa imempa nafasi Kiongera ambaye sasa yuko kwenye kambi ya Harambee Stars inayojiandaa na michuano ya Kombe la Mataifa Afrika.
Taarifa zimeeleza Simba inaendelea na kusaka wachezaji nchini Nigeria ili kuziba bafasi hiyo aliyokuwa apewe Kiongera anayesifika kwa mashuti makali na mipira ya vichwa.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA

Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...

TIBA YA KIIMANI

TIBA YA KIIMANI

a

a
Adbox