Mshambuliaji Dani van Wyk kulia akimtoka beki Mohammed Hussein 'Tshabalala' mazoezini leo Chuo Kikuu |
MSHAMBULIAJI wa zamani wa SuperSport United ya Afrika Kusini, Dani van Wyk ametua Simba SC kwa ajili ya majaribio na kocha Mcroatia, Zdravko Logarusic amesema anahitaji muda zaidi kumuona.
Simba SC imeanza rasmi mazoezi leo Uwanja wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na Logarusic amesema mshambuliaji huyo ameonyesha anaweza, ila anahitaji muda zaidi kabla ya kuamua kumsajili au la.
Mwenyewe van Wyk amesema anaamini atafuzu majaribio Simba SC na akisajiliwa ataisaidia timu hiyo kutokana na uzoefu wake.
“Nina
furaha kuwa hapa, naamini nitafanya vizuri na kumvutia kocha, najua
nikipata nafasi hapa nitaisaidia Simba SC, hii ni timu kubwa na
inahitaji wachezaji wenye uwezo na wazoefu,”amesema.
Mshambuliaji huyo amesema amewahi pia kucheza
Durban FC ya Afrika Kusini kabla ya kwenda kucheza Malaysia.
Wachezaji wengine wapya waliotua mazoezini Simba SC leo ni kipa Hussein Sharrif ‘Cassilas’ kutoka Mtibwa Sugar, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’ kutoka Kagera Sugar na mshambuliaji Michael Mgimwa kutoka Thailand, ambaye aliibukia Taasisi ya Soka Tanzania (TSA), iliyoibua nyota wengine kadhaa akiwemo Thomas Ulimwengu.
Simba SC imeanza mapema maandalizi ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, inayotarajiwa kunaza Septemba 20 mwaka huu.

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni