UEFA imetoa Adhabu ya Kifungo cha Mechi moja kwa Kocha wa Atletico
Madrid Diego Simeone na Kiungo wa Real Madrid Xabi Alonso kwa utovu wa
nidhamu wakati wa Fainali ya UEFA CHAMPIONS LIGI Msimu uliopita.
Fainali hiyo ilichezwa huko Lisbon, Ureno hapo Mei 24 na Real kutwaa Ubingwa wa Ulaya baada ya kuinyuka Atletico 4-1 katika Dakika 120 za Mchezo.
Simeone aliadhibiwa kwa kuvamia Uwanja mwishoni mwa Mechi na kuanza kubatukiana na Sentahafu wa Real Madrid Raphael Varane.
Simeone atatumikia Kfungo chake cha Mechi moja kwenye Mechi inayofuata ya Ulaya ambayo ni Mechi ya Makundi ya UEFA CHAMPIONS LIGI Mwezi Septemba kwani Atletico Madrid wamefuzu kucheza hatua hiyo kwa vile ni Mabingwa wa Spain.
Xabi Alonso aliadhibiwa kwa utovu wa nidhamu kutokana na kuleta rabsha pembeni mwa Uwanja wakati yeye hakuwa Mchezaji kwa vile alikuwa kwenye Kifungo cha
Mechi moja.
Alonso atatumikia Adhabu yake kwenye Mechi ya UEFA Super Cup kati ya Real Madrid na Washindi wa Europa Ligi, Sevilla, itakayochezwa Agosti 12 huko Cardiff, Wales.
Mbali ya Adhabu hizo kwa Wachezaji, kila Klabu, Real na Atletico, zimeadhibiwa kwa utovu wa nidhamu kwa kuwa kila Timu ilizoa zaidi ya Kadi za Njano 5 kwenye Mechi.
Real walipewa Kadi 5 na kupigwa Faini Euro 18,000 wakati Atletico, waliozoa Kadi 7, wamepigwa Faini Euro 21,000.
Vile vile, UEFA imezionya Klabu zote mbili kutokana na Mashabiki wao kufyatua Fataki ndani ya Uwanja wakati wa Fainali hiyo.

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni