Arsene Wenger anahitaji kuona vijana wake wanacheza kwa kiwango cha juu zaidi tofauti na mechi ya Palace.
KWA aliyeangalia kwa umakini mazoezi ya Asernal chini ya kocha Aserne Wenger kwa siku mbili wamekuwa wakijifua barabara ili kuepuka kusubiri dakika za lala salama kupata ushindi.
KWA aliyeangalia kwa umakini mazoezi ya Asernal chini ya kocha Aserne Wenger kwa siku mbili wamekuwa wakijifua barabara ili kuepuka kusubiri dakika za lala salama kupata ushindi.
Jumamosi iliyopita Aaron Ramsey aliiokoa
Asernal sekunde za mwishoni katika mchezo wa ufunguzi wa ligi kuu
England na kushinda mabao 2-1 dhidi ya Crystal Palace katika uwanja wa
Emirates.
Jana jumatatu, Aserne Wenger aliwasili
mjini Istanbull nchini Uturuki kwa ajili ya mechi ya mtoana ya ligi ya
mabingwa barani Ulaya dhidi ya Besiktas leo jumanne.
Wenger akizungumza na wachezaji wake kuelekea mechi ya ligi ya mabingwa dhidi ya Besiktas
Wenger hakufurahishwa na kiwango cha
timu yake dhidi ya Palace, ambapo ilimchukua dakika nyingi kupata bao la
ushindi na kusubiri sekunde chache kabla ya mpira kumalizika ambapo
Ramsey aliandika goli la ushindi.
Kuelekea mechi ya leo usiku, Wenger anahitaji kuona timu inacheza kwa kiwango cha juu na kupata mabao ya mapema.
"Hatuna furaha kabisa kwa kiwango chetu
cha mechi iliyopita jumamosi na tunatakiwa kujiboresha," alisema. "Ni
kipimo kikubwa kwetu. Tuna maandalizi ya muda mfupi na tunajua kwa wiki
moja tuna mechi tatu ngumu dhidi ya Besiktas nyumbani na ugenini na katikati tuna mechi na Everton. Tunatakiwa kukaza buti"
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni