Manchester United
walipoteza kwa mabao 2-1 mechi ya ufunguzi, ligi kuu nchini England
dhidi ya Swansea katika uwanja wa Old Trafford.
MANCHESTER United ipo hatarini kuingia
katika mgogoro tena baada ya mashabiki waliokosa uvumilivu kupanga
kufanya maandamamo makubwa wakipinga kitendo cha wamiliki wa klabu hiyo,
Familia ya Glazer kushindwa kuwekeza katika kikosi.
Mashabiki hao wanashinikiza wamiliki kuondoka Old Trafford kama watashindwa kusajili nyota wapya.
Zikisalia siku 10 dirisha la kiangazi la
usajili kufungwa, Lous Van Gaal bado ana kikosi dhaifu na anahitaji
kusajili ili kuingia katika ushindani wa ligi kuu.
Makama mwenyekiti wa klabu hiyo Ed
Woodward bado ana matumaini ya kukamilisha usajili wa beki wa kati wa
Sporting Lisbon, Marcos Rojo, wakati huo huo akiamnini kuwa wataweza
kumshawishi Angel di Maria kutua Old Trafford kutokea klabu yake ya sasa
ya Real Madrid.
Pia wanamhitaji beki wa Ajax ya Uholanzi, Daley Blind
Mashabiki hawana furaha: Sehemu ya mashabiki wa Man United wanaoweza kuandamana dhidi ya familia ya Glazer kwenye mechi na QPR
Mashabiki wa Manchester United hawana furaha na wamiliki wa klabu hiyo, familia ya Glazer
Hali ngumu: Louis van Gaal anajua kuwa anahitaji kuongeza wachezaji kabla ya dirisha la usajili kufungwa.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni