STAY WITH US

LightBlog

Breaking

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

TANGAZA NASI: +255 655 442 255

CHANZI OPEN SCHOOL

CHANZI OPEN SCHOOL

Jumanne, 19 Agosti 2014

ALIYEKUWA KOCHA WA YANGA ATUA RASMI COASTAL UNION

Razack Siwa (kushoto) akiwa na aliyekuwa kocha wa zamani wa Yanga, Mholanzi, Ernie Brandits


ALIYEKUWA Kocha wa makipa wa timu ya Yanga Razack Siwa  hatimaye

ameingia mkataba wa kuwanoa makipa wa timu ya Coastal Union ya Tanga ambayo inajiandaa na maandalizi ya msimu ujao wa Ligi kuu Tanzania bara utakaoanza Mwezi ujao hapa nchini
.

Siwa ameingia mkataba wa mwaka mmoja lengo likiwa kuipa mafanikio makubwa timu hiyo msimu ujao.

Tayari Kocha Siwa ameungana na wachezaji wa timu hiyo leo kupanda ndege kuelekea Visiwani Pemba ambapo timu hiyo inakwenda kuweka kambi ikijiwinda na michuano ya Ligi kuu soka Tanzania bara.

Akizungumza kabla ya timu hiyo kuondoka  ,Katibu Mkuu wa Coastal Union ,Kassim El Siagi amesema kuwa kocha huyo wa makipa anachukua nafasi iliyokuwa wazi kutokana na kutokuwa na mwalimu maalumu wa kuwafundisha walinda milango wa Coastal Union.

Akizungumzia safari ya timu hiyo, El Siagi alisema kuwa safari ya timu hiyo leo wameondoka  wachezaji 27 wakiaambana na walimu wa timu hiyo ambao wameondoka ambapo watakapofika pemba watafanya mazoezi kwenye uwanja wa soka Gombani.
Safari hiyo imefadhiliwa na wadhamini wa timu hiyo kiwanda cha Pemba Floor Mils kilichopo mjini Tanga ambao wamedhamiria kuhakikisha wanaipa mafanikio timu hiyo.
Katibu huyo amesema wakiwa visiwani humo watacheza mechi nne za majaribio ambazo zilikwisha kutayarishwa na chama cha mpira wa miguu Pemba pamoja na kuwataka mashabiki na wapenzi wa timu hiyo kuacha kuwa na wasiwasi na timu hiyo kwa sababu wamefanya usajili wa nguvu .

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

KAMATI YA TUZO IMEFANYA MCHUJO KWENYE WACHEZAJI 30 WAMEBAKI 15, MKUDE, AJIBU WAMETOLEWA, ANGALIA ORODHA

Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), iliyokutana wiki hii imeteua wachezaji 15 kwa ajili ya kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL msi...

TIBA YA KIIMANI

TIBA YA KIIMANI

a

a
Adbox