Na Boniface Wambura, Dar es salaam
Timu
za Mtibwa Sugar na Polisi Morogoro zinazojiandaa na Ligi Kuu ya Vodacom
(VPL) zitacheza Jumamosi (Agosti 23 mwaka huu) mechi ya majaribio ya
mfumo wa tiketi za elektroniki.
Mechi hiyo itafanyika kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro kuanzia saa 10 jioni wakati kiingilio kitakuwa sh. 1,000.
Tiketi
za mechi hiyo zitaanza kuuzwa kesho (Agosti 20 mwaka huu) kupitia
mtandao wa M-Pesa, CRDB Simbanking na maduka 30 ya Fahari Huduma
yaliyopo katika wilaya zote za Mkoa wa Morogoro, wengi wao wakiwa
Morogoro Mjini.
Washabiki 100 wa kwanza kuingia uwanjani wapata jezi za timu za Mtibwa Sugar na Polisi.
Tayari
mechi ya majaribio ya tiketi za elektroniki imeshafanyika kwenye Uwanja
wa Kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya ambapo timu za Tanzania Prisons
na Mbeya City zilipambana na kutoka sare.
Mechi
nyingine za majaribio ya tiketi za elektroniki zitachezwa Agosti 30
mwaka huu. Uwanja wa Mkwakwani jijini utakuwa na mechi kati ya Coastal
Union na Mgambo Shooting wakati katika Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba ni
Kagera Sugar dhidi ya mabingwa wa Mkoa wa Kagera, Eleven Stars.
Septemba
6 mwaka huu katika Uwanja wa Taifa kutakuwa na mechi kati ya Simba na
Mtibwa Sugar. Mechi nyingine ni ya Ngao ya Jamii kati ya Azam na Yanga
itakayofanyika Septemba 13 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni