Mhaiti, Leonel Saint-Prexu (kushoto) amekosa penalti.
MABINGWA wa Tanzania,
Azam fc wametupwa nje ya michuano ya kombe la klabu bingwa Afrika Mashariki na
kati, Kombe la Kagame kwa kufungwa penalty 4-3 dhidi ya El Merreik ya Sudan katika mchezo wa robo fainali.
Mshindi wa mchezo
huo uliopigwa katika dimba la Nyamirambo mjini Kigali, Rwanda, alilazimika
kupatikana kwa changamoto ya matuta baada ya dakika 90 kumalizika kwa suluhu ya
bila kufungana (0-0).
Mechi hiyo ilikuwa
ngumu kwa timu zote kwani mashambulizi ya kupangwa yalitawala kwa pande zote.
Azam walikosa nafasi
kadhaa za kufunga kupitia kwa washambulaiji wake,Kipre Herman Tchetche, John
Bocco na Leonel Saint-Prexu, lakini nao Merreikh ambao wana historia kubwa
katika soka la ukanda huu walishindwa kuzitumia vizuri nafasi walizopata.
Hata hivyo huwezi
kuacha kumsifu kipa wa Azam fc, Mwadini Ali kwasabbau aliokoa michomo ya hatari
langoni mwake ambayo ilikaribia kuingia nyavuni.
Penati tatu za Azam
fc zilifungwa na beki wa kati Aggrey Morris, mshambuliaji alitokea benchi,
Mrundi, Didier Kavumbagu na Erasto Edward Nyoni.
Beki wa kulia Shomari
Salum Kapombe na Mshambulaiji, Mhaiti, Leonel Saint- Prexu alikosa penalti
yake.
Kwa matokeo haya,
Azam fc kesho wanasafiri kurudi Dar es salaam Tanzania,wakati Merreikh
wanamsubiri mshindi wa mechi ya pili inayoendelea muda huu baina ya KCC ya
Uganda na Altabara ya Sudan kusini.
Nusu fainali moja
imeshajulikana ambapo timu mbili za Rwanda, Polisi na APR zitachuana baada ya
kushinda kwa penalti pia katika michezo ya jana.
Polisi waliifunga Atletico kwa penati 9 kwa 8, wakati APR waliitoka Rayon Sport kwa penalti 4 kwa 3.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni