Amefungua akaunti: Rodriguez akishangilia bao lake na wachezaji wenzake wa Real Madrid
MFUNGAJI bora wa kombe la dunia lililomalizika majira haya ya kiangazi nchini Brazil, James
Rodriguez alifunga bao lake la kwanza Real Madrid, lakini halikuweza
kuipa ushindi timu hiyo ya Carlo Ancelotti dhidi ya Atletico Madrid
katika mchezo wa kwanza wa Super Cup.
Raul Garcia aliisawazishia Atletico kwa kuunganisha mpira wa kona zikiwa zimesalia dakika tatu tu mpira kumalizika.
Real wangeweza kushinda baada ya kufanya
shambulizi hatari dakika za mwisho, lakini Mario Suarez aliweza kuzuia
shuti lililopigwa na Dani Dani Carvajal.
Katika mchezo huo, mshambuliaji tegemeo
wa klabu hiyo, Mreno, Cristiano Ronaldo alitolewa nje wakati wa
mapumziko na kumpisha Rodriguez. Madrid.
Ni mimi! Raul Garcia (kushoto) akishangalia baada ya kuisawazishia Atletico Madrid katika dimba la Bernabeu
James Rodriguez alijiunga na Real Madrid kutokea klabu ya Monaco majira haya ya kiangazi kwa dau la paundi milioni 60
Hofu: Cristiano Ronaldo akishika mgongo wake kabla ya kutolewa na nafasi yake kuchukuliwa na Rodriguez baada ya mapumziko.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni