JOSE
Mourinho amesisitiza kuwa anahitaji kumbakisha kipa wake Petr Cech katika klabu
ya Chelsea, licha ya kumuanzisha Thibaut Courtois kwenye mechi ya ufunguzi wa
ligi kuu England jana usiku dhidi ya Burnley ambapo alishinda kwa mabao 3-0.
Cech
amekuwa akihusishwa kujiunga na klabu mbalimbali zikiwemo PSG na Real Madrid,
kufuatia kurejea kwa Courtois aliyecheza kwa mkopo kwa misimu mitatu katika
klabu ya Atletico Madrid.
Lakini
inafahamika kuwa Chelsea wapo tayari kusikiliza ofa nzuri juu ya kipa huyo
mwenye miaka 32.
“Naamini
hakuna mtu atakayekuja na naamini ninachokisema, naweza kuwa na makipa bora
watatu na itakuwa nzuri sana,” aliwaambia Sky Sports.
“Lakini
heshima ya kwanza ni kumbakisha klabuni kwasababu tunahitaji makipa wa kiwango
cha juu, jumlisha Mark (Schwarzer) ambaye ni kipa mkubwa”.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni