MARCOS Rojo amethibitisha kukamilisha usajili wake kujiunga na Manchester United
akitokea klabu ya Sporting Lisbon na kusisitiza kuwa ndoto ya kucheza ligi kuu
Egland imetimia.
Inafahamika
kuwa mashetani wekundu wamekubali kutoa paundi milioni 20 ili kumnasa Muargentina
huyo, huku Luis Nani akijiunga kwa mkopo katika misingi mingine.
“Nahisi
kama ni ndoto kuwa mchezaji wa Manchester United,” Beki huyo aliwaambia ARV Radio Continental. “Kuondoka
Sporting Lisbon haikuwa rahisi”.
Siku
chache zilizopita Rojo alitawala kwenye vyombo vya habari baada ya kuondoka
katika mazoezi ya Sporting kufuatia klabu hiyo kukataa ofa ya United, lakini
aliwaomba radhi wachezaji na mashabiki kwa kitendo hicho kisichokuwa cha
kiungwana.
Beki
huyo mwenye miaka 24 alifika fainali ya kombe la dunia akiwa na nchi yake ya
Argentina na kufungwa bao 1-0 dhidi ya Ujerumani.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni