Mashambulizi: Bosi wa Chelsea, Jose Mourinho imezipasha timu mbili pinzani katika mbio za kuwania ubingwa .
JOSE Mourinho kama kawaida amezipasha
Asernal na Manchester City, moja ya timu pinzani katika mbio zake za
kuwania ubingwa msimu mpya unaonza leo.
Kocha huyo wa Chelsea alishindwa kutwaa
kombe lolote katika msimu wake wa kwanza baada ya kurudi mwaka jana,
wakati Aserne Wenger alimaliza ukame wa miaka tisa bila kikombe baada ya
kushinda kombe la FA.
Alipoulizwa kama anajisikia presha
yoyote juu ya kufanikiwa kutwaa ubingwa, Mourinho alisema: "Kwanini?
baadhi ya makocha imewachukua miaka 10 kushinda kombe."
Manuel Pellegrini alishinda taji la ligi na kombe la ligi msimu uliopita akiwa na kikosi cha kurithi kutoka kwa Roberto Mancini.
Chini ya Muitaliano huyo Man City walishinda taji la ligi kuu, kombe la FA na Ngao ya Hisani.
Mourinho aliongeza: "Sipendi kuona klabu
inaendelea chini ya kocha mwingine kabla yangu, sitaki kufika wakati
ambao navuna matunda kwenye miti yao. Napenda kufanya kazi. Napenda
kujenga. Sipendi kazi nyepesi."
Mourinho hataki kujipa presha licha ya kushindwa kutwaa taji msimu uliopita
Msimu uliopita, Mourinho alimuita Aserne Wenger 'Bingwa wa kushindwa' na alimchana Pellegrini kuwa alitumia fedha nyingi zaidi.
Mreno huyo anajiona kuwa yupo katika
mchakato wa kujenga kikosi chake Stamford Bridge na sio kutumia kile
alichoachiwa na Rafael Benitez.
Majira haya ya kiangazi amemleta Diego
Costa kwa paundi milioni 32 na kutumia paundi milioni 16 kumsajili Filep
Luis, wote kutoka Atletico Madrid.
Pia alimsajili Cesc Fabregas kutoka Barcelona kwa paundi milioni 30 na kumuongeza Didier Drogba aliyekuwa mchezaji huru.
Kocha wa Arsenal, Arsene Wenger alimaliza ukame wa kutoshinda taji kwa miaka 9 baada ya kutwaa FA mwezi mei mwaka huu.
"Huu ni mwaka pili katika mpango wangu
na nina furaha na hilo,' alisema Mourinho. 'Mwishoni mwa msimu ninyi,
mashabiki na wachezaji wataipima kazi yangu. Na muhimu zaidi na bosi
wangu, mmiliki na Bodi itapima kazi yangu'.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni