Nyota anayechipukia: Thibaut Courtois anatazamiwa kuanza dhidi ya Burnley.
THIBAUT Courtois ameshinda mbio za kuwa kipa namba moja wa Chelsea.
Mbelgiji huyo anatazamiwa kuanza mbele ya Petr Cech katika mchezo wa ufunguzi wa ligi kuu jumatatu usiku dhidi ya Burnley.
Bingwa: Courtois (katikati) alishinda La Liga akiwa na Atletico Madrid msimu uliopita.
Paris Saint-Germain, Monaco na Real Madrid wote wanaonekana kuwa na nia ya kumsajili Cech.
Wanasubiri kuona maamuzi ya Mourinho ili kuanza harakati za kumnasa kipa huyo.
Courtois alikuwa akicheza kwa mkopo kwa
misimu mitatu iliyopita katika klabu ya Atletico Madrid na alikuwa
sehemu ya kikosi kilichozishangaza Real madrid na Barcelona na kutwaa
ubingwa wa La Liga na kufika fainali ya UEFA.
Cech amekuwa kipa namba moja wa Chelsea tangu ajiunge na klabu hiyo mwaka 2004.
Mourinho anaamini atawatumia makipa wote
katika kampeni zake, lakini alikiri ijumaa kwamba mchezaji
asipochaguliwa kama namba moja katika kikosi chake anatakiwa kuanza
kuangalia hatima yake ya baadaye klabuni hapo.
Cech mwenye miaka 32 anaweza kuamua
kukaa benchi katika mechi nyingi za msimu au kutafuta ukurasa mpya wa
maisha yake ya soka katika klabu nyingine
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni