KIUNGO wa Manchester United, Ander Herrera amesema
yeye na wachezaji wenzake wana malengo ya kuirudisha klabu hiyo nafasi ya juu
katika soka la Ulaya.
Baada ya kumaliza katika nafasi ya saba msimu
uliopita, United wanaanza kampeni za kusaka ubingwa wa England bila kushiriki
michuano ya Ulaya kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1989-90.
Herrera ambaye alijiunga na United baada ya
kuanguka mwaka 2013, anasisitiza kuwa kikosi cha Louis Van Gaal kinajipanga
kufuta machungu ya msimu uliopita.
“Nisingeweza kuondoka Athletico kama nisingejiunga
na klabu kama United,” Herrera aliwaambia The
Guardian. “United ni fursa nzuri ambayo huwezi kukataa”.
“Niliiacha klabu ya kipekee, yenye falsafa maalumu
na watu maalumu”
“Ni klabu ambayo wachache tunajivunia kuichezea,
lakini kwa United naweza kukaa kwa miaka 10”.
“Hii ni klabu kubwa England, mpango mpya,
wachezaji wapya na kocha mpya”
Herrera anatazamiwa kuanza mechi yake ya kwanza ya ligi kuu dhidi ya Swansea City leo jumamosi katika dimba la Old Trafford.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni