Kazi imeanza: Luis Suarez
akifanya mazoezi na wachezaji wenzake wa Barcelona leo ijumaa akiwemo
nahodha wa klabu, Xavi.
BAADA ya kuanza mazoezi na wachezaji wenzake wa
Barcelona kwa mara ya kwanza jana ijumaa, Luis Suarez amesema ni muda wa
kusahau miezi miwili iliyopita.
Siku ya Alhamis, mahakama ya juu ya rufani ya
michezo ya CAS alitangaza kuwa kifungo cha miezi minne cha Luis Suarez kujihusisha
na shughuli za michezo kisijumuishe na kutoshiriki mazoezi.
FIFA walimfungia Muuruguay huyo baada ya kumng’ata
beki wa Italia, Giorgio Chiellin katika fainali za kombe la dunia-na hii
ilikuwa mara ya tatu kukutwa na hatia ya kosa la aina hiyo.
Mshambuliaji huyo aliyejiunga na Barcelona
akitokea Liverpool kwa dau la paundi milioni 75 alianza mazoezni na kikosi cha
Barcelona ijumaa na anaweza kucheza mechi ya kwanza siku ya jumatatu katika
mechi ya kirafiki dhidi ya Leon kwenye uwanja wa Camp Nou.
“Nina furaha kubwa ya kucheza tena mpira na
wachezaji wenzangu,” Suarez aliiambia Tovuti ya Barca.
“Hali ya kutocheza ilinikosesha raha. Ninajutia
makosa niliyoyafanya na niliomba msamaha, lakini haya yasahaulike”.
“Tufikirie ya baadaye katika klabu yangu ya Barcelona, klabu niliyoota kuichezea”.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni