KLABU ya Benfica imekamilisha usajili wa kipa wa kimataifa wa Brazil, Julio Cesar kwa mkataba wa miaka miwili kutoka QPR.
Mlinda mlango
huyo mkongwe mwenye umri wa miaka 34 alijiunga na klabu hiyo ya London
mwaka 2012, lakini akacheza mechi 24 kabla ya kwenda kwa mkopo Toronto.
Robert
Green amechukua nafasi yake kama kipa wa kwanza wa klabu hiyo na
Benfica imeamua kumchukua kipa huyo aliidakia Brazil iliyofanya vibaya
Kombe la Dunia mwaka huu.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni