Straika wa Azam FC, Mrundi, Didier Kavumbagu ameweka wazi kuwa, anatumia vidonge maalum
kuongeza virutubisho vya mwili ambavyo vinamsaidia kuwa mwepesi na kumudu
programu za kocha wake.
Kavumbagu
ambaye alikipiga Yanga misimu miwili kwa mafanikio aliyasema hayo hivi
karibuni ambapo alikiri kuwa vidonge hivyo vinaongeza
virutubisho muhimu mwilini, pia kuulainisha mwili kuwa tayari kwa ajili
ya
mazoezi magumu ya kimichezo na si vinginevyo.
“Nimefanya
vizuri katika mazoezi kwa kuwa ninapata muda mwingi wa kupumzika na kula
chakula katika muda mwafaka, pia kuna rafiki yangu yupo Ulaya amenitumia
vidonge f’lani vya vitamin ambavyo nikimeza vinaufanya mwili uwe huru na kuwa
tayari kwa ajili ya mazoezi.
“Ni
vidonge vya kawaida ambavyo mwanamichezo yeyote anaweza kutumia bila ya kupata
madhara, hata Didier Drogba wa Chelsea anavitumia sana,” alisema Kavumbagu.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni