Mbwana Samatta (kushoto) na Thomas Ulimwengu (kulia)
WASHAMBULIAJI wawili wa kimataifa wa
Tanzania wanaokipiga TP Mazembe ya DR Congo, Mbwana Ally Samatta na Thomas
Emmanuel Ulimwengu wataiongoza klabu yao dhidi ya mahasimu wao wa jadi, AS Vita katika mchezo wa mwisho wa kundi A wa
ligi ya mabingwa barani Afrika.
Kuelekea katika mechi hiyo
atakayochezwa mjini Kinshasa, homa imepanda kwa mashabiki wa klabu hizo ingawa zote zimefuzu kucheza
nusu fainali, lakini heshima ndio kitu muhimu zaidi.
Mechi hiyo itaamua ni klabu gani imalize
ya kwanza kundi A ambapo ni mara ya kwanza katika historia ya DR Congo kuona
klabu mbili za nchi hiyo zikifuzu hatua ya nusu fainali ya ligi ya mabingwa.
Kitu cha pili, AS Vita wanataka
kuhakikisha wanashinda dhidi ya Mazembe ili kuwapa raha mashabiki wake
kwasababu wamefungwa mara mbili mfululizo.
Mazembe wanarudi katika dimba la
Stade Tata Raphael ikiwa imepita miezi minne tangu waifunge Vita 1-0, mei 11
mwaka huu na kutwaa ubingwa wa ligi kuu, lakini kulitokea vurugu kubwa na
kusababisha watu 15 kupoteza maisha.
Wakati huo huo Mazembe wanajipanga
kuibuka na ushindi wa tatu mfululizo dhidi ya AS Vita ili kumaliza kileleni
katika kundi A na kucheza nusu fainali mwezi septemba.
Hata hivyo, wanakabiliana na Vita ambao wamepoteza mechi moja tu katika kundi A na wanakwenda kucheza mechi hiyo wakitokea kushinda bao 1-0 ugenini dhidi ya waburuza mkia wa kundi hilo, Zamalek, Agosti 10 mwaka huu.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni