Angel Di Maria (kushoto) na Sami Khedira wanatakiwa na Manchester United.
MANCHESTER United bado wanapambana
kuhakikisha wanawasajili nyota wawili wa Real Madrid, Muargentina, Angel
di Maria na Mjerumani Sami Khedira.
Habari njema kwa mashabiki wa United ni
kwamba makamu mwenyekiti wa klabu hiyo, Ed Woodward anapigana kuwasajili
wachezaji hao kabla ya kufungwa kwa dirisha la usajili.
Di Maria amekuwa katika rada za Louis
Van Gaal kwa majira yote ya kiangazi wakati Khedira alimuona wakati
anafundisha soka nchini Ujerumani.
Anawindwa: Di Maria ndiye chaguo namba moja la Louis van Gaal na Manchester United majira haya ya kiangazi.
Milango wazi: Carlo Ancelotti alisema
'kama Di Maria hatapata suluhisho la hatima yake ya baadaye, kwa furaha
tutapenda kumkaribisha tena.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni