MARSEILLE walifungua vibaya uwanja wa Stade Velodrome baada ya
kuchapwa na wageni Montpellier.
Rais wa UEFA, Michel Platini alikuwepo katika uwanja huo, lakini
ni mechi ambayo wenyeji kamwe hawataisahau.
Kupoteza mabao 2-0 dhidi ya Montpellier yalikuwa matokeo mabaya na
hali ya kisanga cha Andre Ayew kilibaki kuwa gumzo uwanjani.
Nyota huyo wa Ghana katika fainali za kombe la dunia majira ya
kiangazi mwaka huu nchini Brazil, alipata majeraha kichwani kipindi cha kwanza
na ilimlazimu kubadilisha jezi baada ya damu kutawala katika jezi yake na
aliendelea na mechi.
aliendelea na mechi.
Kipindi cha pili, bandeji katika jeraha hilo ilitoka na damu
kuanza kutoka na kuchafua jezi yake na ikambidi abadili tena. Lakini kulikuwa
na tatizo.
Marseille walikuwa na jezi zake mbili tu namba 10 mgongoni na
yatari alikuwa ameshazichafua zote kwa damu.
Ayew alionekana katika TV ya uwanjani akiwa amechukizwa na kitendo hicho
Mtunza vifaa wa klabu hiyo alitoa jezi namba 33, lakini kwa kuwa
Ayew alianza mechi kwa kuvaa jezi namba 10, alitakiwa kumaliza mechi kwa namba
hiyo hiyo.
Kwahiyo, timu ilijaribu kufuta namba 33 na kuandika namba 10, lakini
jitihada ziligonga mwamba, kwahiyo Marseille ikabidi wamtoe Ayew katika dakika
ya 52 baada ya kukosa jezi. Hali hii ilimchefua sana kocha Marcelo Bielsa.
Hakuna aliyemtia moyo, Ayew alirudi benchi akiwa hana jezi yoyote.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni