MSHAMBULIAJI nyota wa
klabu ya Barcelona, Luis Suarez amesema mazungumza na mtaalam kuhusu
tabia yake na kusisitiza kuwa hatafanya tukio kama hilo tena.
Suarez
kwasasa anatumikia adhabu ya kufungiwa miezi minne kwa kung’ata beki wa
Italia Giorgio Chiellini katika michuano ya Kombe la Dunia likiwa ni
tukio lake la tatu.
Nyota huyo wa kimataifa wa Uruguay amesema kuwa
amezungumza na daktari wake wa ushauri na akamwelekeza inabidi akubali
kosa na kuomba radhi suala ambalo amefanya na sasa anaganga
yajao.
Suarez mwenye umri wa miaka 27 amesema alipatwa na huzuni baada
ya tukio alilofanya nchini Brazil lakini anashukuru suala hilo kwasasa
liko nyuma yake na anasonga mbele kuona jinsi atakavyoisaidia timu yake
mpya wa Barcelona.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni