MAHAKAMA ya Kimataifa ya
Usluhishi wa Michezo, CAS imetupilia mbali rufani ya kupunguziwa adhabu
ya mshambuliaji nyota wa kimataifa wa Uruguay Luis Suarez lakini
ameruhusiwa kufanya mazoezi na timu yake mpya ya Barcelona.
Mawakili wa
Suarez walikata rufani CAS kupinga uamuzi wa Shirikisho la Soka
Duniani-FIFA kumfungia mteja wao miezi minne kujishughulisha na mambo ya
michezo kwa kosa la kumng’ata Giorgio Chiellini katika michuano ya
Kombe la Dunia.
Sasa mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 27 ambaye
atamaliza adhabu yake Octoba 25 ataweza kucheza mechi yake ya kwanza
katika mchezo wa El Clasico wakati Barcelona watakapokuwa wageni wa Real
Madrid Octoba 26 mwaka huu.
Nyota huyo pia ataendelea kuitumikia adhabu
yake ya mechi tisa za kimataifa kama kawaida lakini sasa masharti
yamelegezwa kidogo kwani anaweza kufanya mazoezi na wenzake na pia
kuhudhuria mechi.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni