Katika michuano hiyo inayodhaminiwa na Capital One, ikienda kwa jina la Capital One Cup ambayo mabingwa wa mwaka jana ni Manchester City, United wamepangwa kucheza na Milton Keynes Dons, maarufu kama MK Dons.
Mara ya mwisho kuanza kwenye hatua hii ya awali ilikuwa Septemba 1995 ambapo Manchester United walikandikwa 4-3 na York. Timu nyingine zinazoshiriki katika hatua hii ni pamoja na Bradford, Leeds, Newcastle, Gillingham, Stoke na Portsmouth.
Mechi za hatua hiyo zimepangwa kuchezwa wiki inayoanza Aprili 24.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni