United wapo tayari kumruhusu Nani (kulia) kujiunga na Sporting Lisbon kama sehemu ya kubadilishana na beki Marcos Rojo.
MANCHESTER United imefanya mazungumzo na
Sporting Lisbon ili kumjumuisha Luis Nani kama sehemu ya jaribio la
kutaka kumsajili beki wake, raia wa Argentina, Marcos Rojo.
Baada ya mazungumzo baina ya wakala wa Rojo na Sporting mapema wiki hii, United wanajiandaa kumjumuisha Nani kwa mkopo.
Hata hivyo winga huyo mwenye miaka 27 anaonekana kuweka ngumu kurudi katika klabu yake hiyo ya zamani ya nchini Ureno.
Sporting wao wanahitaji kumuuza Rojo kwa paundi milioni 24, lakini wiki hii Man United waliweka mezani dau la paundi milioni 16.
Rojo, 24, aliwaomba radhi mashabiki wa
Sporting katika mahojiano maalumu na TV ya klabu jumapili usiku baada ya
kujaribu kulazimisha kuondoka.
Msamaha: Rojo aliwaomba radhi mashabiki wa Sporting Lisbon
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni