Manuel Pellegrini anaamini kikosi chake cha ubingwa kimeimarika zaidi kwa kipindi chake cha mwaka mmoja.
Mabingwa hao watetezi wa ligi kuu England walizindua kampeni zao za EPL kwa kuitandika Newcastle United mabao 2-0 jana jumapili.
Pellegrini alifurahishwa na ushindi huo licha ya wachezaji wake wengi waliocheza kombe la dunia kutokuwa fiti ipasavyo.
Lakini anajua kuwa kutakuwa na ushindani
mkubwa kwa mara nyingine tena msimu huu, ila ameonya kuwa kikosi chake
kimeimarika zaidi chini yake.
Mabingwa: Manuel Pellegrini alishinda taji la ligi kuu England msimu uliopita.
Alisema: "Ni ngumu sana kufananisha kila
mwaka. Labda msimu uliopita watu wengi walinihofia kuwa sitaweza kutwaa
ubingwa kwasababu ulikuwa msimu wangu wa kwanza wa ligi kuu England".
"Leo tuna mwaka mmoja tukifanya kazi na kikosi na nadhani pia tuna kikosi bora".
"Lakini siku zote England kuna timu tano
au sita ambazo zinaweza kutwaa ubingwa, hivyo njaa tuliyoanza nayo
katika mechi ya kwanza tunatakiwa kuendelea na wewe"
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni