Marcos Rojo alitua nchini England jana kukamilisha taratibu za usajili katika klabu ya Man United.
MANCHESTER United wamekubali kulipa dau la paundi milioni 16 ili kumsajili beki wa Sporting Lisbon, Marcos Rojo.
Rojo alitua jana jioni mjini Manchester na alisema kujiunga na United "anahisi ni kama ndoto'.
Beki huyo kisiki anatarajia kusaini mkataba wa miaka minne baada ya kufuzu vipimo vya afya na kukubaliana mambo binafsi.
Louis van Gaal ameamua kumsajili beki
huyo kufuatia kipigo cha jumamosi cha mabao 2-1 katika mechi ya ufunguzi
wa ligi kuu England dhidi ya Swansea City.
Karibu kijana: Rojo anajiaunga na United baada ya Sporting Lisbon kukubalia dau la uhamisho.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni