DUNGA ATAJA KIKOSI CHA BRAZIL, ALVES, MARCELO, CESAR, PAULINHO WAPIGWA CHINI...
ANGALIA KIKOSI KAMILI HAPA....
Philippe Coutinho ameitwa kikosi ncha Brazil baada ya kuonesha kiwango kikubwa akiwa na Liverpool.
DUNGA ameanza majukumu yake ya ukocha
mkuu wa timu ya taifa ya Brazil kwa mara ya pili kwa kuwapiga chini
wachezaji 13 walioshiriki fainali za kombe la dunia.
Philippe Coutinho ni miongoni mwa
wachezaji walioitwa kutokana na kiwango kizuri akiwa na Liverpool,
wakati Neymar aliyepona majeruhi yake aliyopata katika fainali za kombe
la dunia naye amejumuishwa katika kikosi hicho.
Amerudi kazini: Dunga bado ina imani na Neymar katika michezo miwili ya kirafiki dhidi ya Colombia na Ecuador.
Ametemwa: Wachezaji wengi wa kikosi kilichoshiriki kombe la dunia akiwemo Julio Cesar, wameachwa na Dunga.
Kipa wa QPR , Julio Cesar, beki wa kulia
wa Barcelona Dani Alves, Marcelo wa Real Madrid na kiungo wa
Tottenham, Paulinho ni miongoni mwa wachezaji wakubwa walioachwa katika
kikosi hicho, wakati nahodha Thiago Silva amekosekana kutokana na
majeruhi.
Dunga alimrithi Luiz Felipe Scolari baada ya kuvurunda katika fainali za kombe la dunia katika ardhi ya Brazil.
Brazil ilifungwa mabao 7-1 na Ujerumani, pia walifungwa mchezo wa mshindi wa tatu na Uholanzi.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni