MTIHANI
wa kwanza wa kocha wa Yanga sc, Brazil, Marcio Maximo ni leo hii ambapo
atawaongoza vijana wa Jangwani kuoneshana ujuzi na timu ya Chipukizi FC ya
Zanzibar.
Maximo
ambaye amekinoa kikosi chake kwa zaidi ya mwezi mmoja tangu arithi mikoba ya Mholanzi,
Hans Van der Pluijm, anatarajia kuwatumia wachezaji wote wa kikosi cha kwanza
na cha pili ili kuona namna walivyopokea mafunzo yake yaliyofanyika kwa muda
mrefu uwanja wa shule ya Sekondari, Loyola, iliyopo Mabibo jijini Dar es
salaam.
Ingawa
mechi hii itakayoanza majira ya saa 10:00 jioni uwanja wa Gombani, Kisiwani
Pemba ni ya kirafiki, lakini ina umuhimu mkubwa kwa Maximo kwasababu anahitaji
kuwaaminisha mashabiki wa Yanga wenye imani kubwa na mwalimu huyu wa zamani wa
timu ya taifa ya Tanzania, ‘Taifa Stars’ (2006-2010).
Viingilio
katika mechi hiyo ni shilingi elfu tatu (3,000/=) kwa VIP na elfu mbili (2,000/=) majukwaa ya kawaida.
Mashabiki
wa Yanga waliopo Pemba na Zanzibar wanatarajiwa kufurika Gombani kuwaona vijana
wa Yanga, hususani Wabrazil wawili, Gleilson Santos Santana ‘Jaja’ na Andrey
Coutinho ambao kwa mara ya kwanza watacheza mechi ya kirafiki tangu wasajiliwe
majira haya ya kiangazi.
Kocha mkuuu Marcio Maximo na kikosi chake
wamefikia katika hoteli ya kitalii ya Pemba Misali iliyopo eneo la Wesha na watajifua
kwa takribani siku 10 kabla ya kurejea jijini Dar es salaam mwishoni mwa mwezi
huu.
Kulingana na program
ya bench la Ufundi kisiwani Pemba, Young Africans inatarajia kucheza michezo
mitatu ya kirafiki na timu za kutoka Visiwa vya Pemba na Unguja na baadaye
kurejea Dar es salaam kwa michezo miwili ya kimataifa kabla ya kucheza mchezo
wa Ngao ya Hisani septemba 13, 2014.
Wachezaji waliopo Pemba
Walinda Mlango Juma
Kaseja, Ally Mustafa "Barthez" na Deogratias Munish "Dida",
Walinzi wa Pembeni, Juma
Abdul, Salum Telea, Oscar Joshua, Edwad Charles na Amos Abel
Walinzi wa Kati ni Kelvin Yondani, Nadir
Haroub "Cannavaro", Rajab Zahir na Pato Ngonyani.
Viungo: Mbuyu Twite, Said Juma
"Makapu", Omega Seme, Hassan Dilunga, Haruna Niyonzima na Hamis
Thabit.
Viungo wa Pembeni: Saimon Msuva, Mrisho
Ngasa, Nizar Khalfani na Andrey Coutinho.
Washambuliaji: Geilson Santos
"Jaja", Said Bahanuzi, Jerson Tegete, Hamis Kizza na Hussein
Javu
Benchi la Ufundi walioko Kisiwani Pemba ni:
Kocha Mkuu : Marcio Maximo
Kocha wasaidizi Leonado Neiva, Salvatory Edward
Kocha wa Makipa: Juma Pondamali
Daktari wa timu: Dr Suphian Juma
Meneja wa timu:
Hafidh Saleh
Mchua Misuli: Jaco Onyango
Mtunza Vifaa: Mahmod Omar "Mpogolo"
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni