Rojo katua : Manchester United wamekamilisha usajili wa Marcos Rojo kutoka Sporting Lisbon.
MANCHESTER United imethibitisha kumsajili beki wa Sporting Lisbon, Marcos Rojo kwa ada ya uhamisho ya paundi milioni 16.
Rojo, aliyewasili mjini Manchester siku
ya jumanne jioni na kusema kujiunga na United "Anahisi kama ndoto'
amesaini mkataba wa miaka mitano baada ya kufuzu vipimo vya afya na
kukubaliana mambo binafsi.
Kipau mbele cha Louis van Gaal ilikuwa
ni kusajili beki wa kushoto na aliamua kubadili mtazamo kwa kumsajili
Rojo mwenye miaka 24 kufuatia kipigo cha jumamosi dhidi ya Swansea City.
Beki huyo raia wa Argentina atavaa jezi namba 5.
Anaingia kikosi cha kwanza: Rojo atavaa jezi namba 5 na amesaini mkataba wa miaka mitano
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni