Anawindwa: Roma wanaitaka saini ya Fernando Torres
ROMA wameulizia uwezekano wa kumsajili mshambuliaji wa Cheslea, Fernando Torres.
Timu hiyo ya Italia, inaitaka saini ya
mshambuliaji huyo wa Hispania, na watawashawishi The Blues kumchukua
Mattia Destro kama sehemu ya dili hilo.
Torres amekuwa na wakati mgumu tangu
ajiunge Stamford Bridge kutokea Liverpool kwa ada kubwa ya uhamisho ya
paundi milioni 50 mwezi januari 2011.
Kocha Jose Mourinho ameongeza wachezaji
katika safu ya ushambuliaji majira haya ya kiangazi ambapo amemsajili
Diego Costa kwa paundi milioni 32 na kumrudisha gwiji wa Chelsea, Didier
Drogba.
Tayari Roma walishamsajili nyota mwingine wa zamani wa Cheslea, beki wa kushoto, Ashley Cole kama mchezaji huru.
Sehemu ya dili: Roma wanataka kuwapatia Mattia Destro kama sehemu ya usajili wa Torres.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni