Majanga: Kiungo wa Arsenal, Mikel Arteta atakaa nje ya uwanja kwa mechi mbili zijazo.
HABARI mbaya kwa mashabiki wa Asernal,
Mikel Arteta atakaa nje ya uwanja katika mechi mbili zijazo baada ya
kupata majeruhi ya kifundo cha mguu wakati wa mechi ya mtoano ligi ya
mabingwa barani Ulaya jumanne ya wiki hii dhidi ya Besiktas.
Nahodha huyo wa Asernal alitolewa katika dakika ya 50 ndani ya dimba la Olympic Ataturk Stadium kufuatia kugongana na mshambuliaji wa zamani wa Cheslea, Demba Ba.
Maumivu: Arteta aliumia kifundo cha mguu.
Arteta atakosa mechi ya jumamosi ya ligi
kuu ugenini dhidi ya Everton na mechi ya marudiano ya ligi ya mabingwa
katika uwanja wa Emirates dhidi ya Besiktas jumanne ijayo.
Nyota huyo atapimwa zaidi leo alhamisi, lakini ni wazi kuwa atakosa mechi mbili zijazo.
Orodha ya majeruhi kwa Asernal tayari imeanza ambapo Yaya Sanogo na Kieran Gibbs walikosa mechi ya suluhu ya bila kufungana mjini Istanbul.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni