Cristian Ronaldo amemzawadia tuzo yake ya mchezaji wa mechi, kocha wake wa zamani, Alex Ferguson.
Ferguson
aliyekuwa kwenye kikosi cha ufundi cha Uefa wakati Real Madrid
ilipowachapa mabingwa Europa Cup, Sevilla 2-0, ndiye aliyeteuliwa
kumkabidhi tuzo hiyo Ronaldo.
Ronaldo alifunga mabao yote mawili katika mechi hiyo iliyopigwa Cardiff.
Manchester United ndiyo iliyomtoa na Ferguson ndiye alimchukua kutoka Sporting Lisbon iliyomkuza kisoka akiwa kinda.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni